Chini ya miaka 40 ni muda mzuri wa kuwekeza na kupata mafanikio kwani unakuwa na nguvu za kufanya mambo makubwa .Tumia mbinu hizi:
ANZA MAPEMA KUWEKA AKIBA NA KUWEKEZA
Usisubiri upate hela nyingi hata elfu tano kila wiki ukiweka baada ya miaka 5 ni mtaji
mkubwa. Wenye umri mdogo wana faida ya
kuwa matajiri kama watawekeza mapema. Usikubali muda upite bila kufanya
kitu kikubwa.
SOMA PIA:Wajue wadukuzi wenye nguvu zaidi waliotikisa Dunia kupitia intaneti
JIFUNZE SKILLS ZENYE THAMANI KUBWA
Badala ya kupoteza muda mwingi kwenye starehe jifunze skills
zinazolipa kama vile:
·
Digital marketing
·
Public speaking
·
Na kutumia AI kutengeneza content
·
Uuzaji<sales>
·
Social media management
Skill moja thamani inaweza kukupa kipato kikubwa kuliko
degree ya kawaida.
JENGA MTANDAO MAPEMA <NETWORKING>
Marafiki zako wa sasa ni wateja au waajiri wa kesho. Kuwa
karibu na watu wenye ndoto kubwa kuliko wewe
watakubeba juu.epuka kuwa na watu wa kawaida kwenye circle yako.
EPUKA MADENI YA KIJINGANA STAREHE.
Usikimbilie mikopo ya simu za gharama kubwa wakati
hazikuingizi kitu mavazi,au lifestyle. Ukiwa mdogo focus ya kwanza ni kujenga
mtaji na biashara kubwa si kuonesha Maisha ya kifahari.
TAFUTA MWALIMU AU MENTOR
Tafuta mtu ambaye atakusimamia njia unayopita. Kila
aliyeweza kufanikiwa ana mtu ambaye
alimpatia mwongozo wa kufanya. Usipoteze miaka 10 ukijaribu kila kitu tafuta
mtu akupe short cut za kweli.
TENGENEZA VYANZO VINGI VYA MAPATO
Usitegemee ajira, kazi au biashara moja uhuru wa kifedha
utapata ukiwa na vyanzo vingi. Hata bahari inakuwa na maji muda wote kwani ina
mifereji mingi ya moto inayoingiza maji. Ndivyo ilivyo utafanikiwa kwa kufanya
hivyo. Kila chanzo kidogo kinajenga nguvu kubwa.
WEKEZA KWENYE AFYA NA NIDHAMU
Mafanikio makubwa yanahitajimwili na akili yenye
nguvu,mazoezi,usingiziwa kutosha na
kuepuka ulevi/ulegevu ni capital kubwa Zaidi kuliko pesa.
Ukijenga nidhamu ukiwa mdogo mafanikio yatakuwa matokeo ya
lazima.
Wengi wanadhani mafanikio ni ya yawazee, lakini ukweli ni
huu ukiwa kijana una advantage
kubwa kuliko mtu yeyote.
Hizi ndizo mbinu zinazokufanya ufanikiwe ukiwa bado mdogo
kuna ambazo tayari unazitumia au ni
jambo gani ambalombado unahitaji usimamizi
kati ya haya?
Niandikie hapo chini kwenye comment ili niweze kukusaidia.
Share ujumbe huu kwa watu wengine ili kuhamasisha mafanikio.